Ministry of Natural Resources and Tourism Community Based Conservation Training Centre (CBCTC) Likuyu Sekamaganga
Community Based Conservation Training Centre (CBCTC) Likuyu Sekamaganga
LMS
SMIS
Mail
Eng
close
close
Head

GESII.jpg

CP: WAKULYAMBA AZINDUA MRADI WA GESI ASILIA CHUO CHA MAFUNZO YA UHIFADHI NA MALIASILI

Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Chuo cha Uhifadhi wa Maliasili kwa Jamii Likuyu Sekamaganga imeendelea kuungwa mkono jitihada za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za uhifadhi wa mazingira kwa kuzindua Mradi wa Gesi asilia itakayotumika chuoni hapo badala ya kutumia kuni

Akizindua Mradi huo wa Gesi asilia Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii anayeshughulikia Maliasili, Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba amesema Wizara hiyo inatekeleza kwa vitendo maono ya Rais Samia katika Uhifadhi wa Mazingira kwa kuhamasisha jamii kutumia nishati safi kwa kupikia na kuachana na matumizi ya nishati ambazo zinaharibu misitu hususani iliyohifadhiwa kisheria.

Wakulyamba amesema mradi huo utasaidia kuondokana na matumizi ya kuni na kutumia nishati mbadala kusaidia kuhifadhi mazingira ya rasilimali za misitu na kuzitaka taasisi nyngine kuiga mfano wa Chuo Cha Uhifadhi wa Maliasili kwa Jamii Likuyu Sekamaganga

"Nimpongeze Mkuu wa chuo hiki Bi. Jane Nyau kwa jitihada zake katika kuunga mkono maono ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan juu ya matumizia ya nishati mbala, niziombe Taasisi nyingine kuiga mfano huu." Amesema CP. Wakulyamba

Rais Samia amekuwa kinara katika ajenda ya Nishati Safi ya Kupikia nchini na Afrika ambapo anaendelea kuipeleka ajenda hiyo Kimataifa ili kuhakikisha watu wanapika katika mazingira salama kiafya na kimazingira.

GESIII.jpg

mgeni rasmi akizindua mradi jiko la gesi.jpg

Posted in News on Dec 19, 2024